Asasi Yetu

FAHAMU ZAIDI JUU YA ASASI YETU YA TAREO

TAREO ni kifupisho cha Tanzania Rural Empowerment Organization ,asasi isiyo  ya kiserikali,kidini wala yenye kutenegeza faida..Tareo iliazishwa mwaka 2000 na kupata usajili mwaka 2008 kwa Sheria ya uazishaji wa asasi zisizo za kiserikali (NGO) No;

Moja ya jukumu letu ni  kuwawezesha wakazi wa vijijini ki-elimu ,Technolojia, Afya na kuwashirikisha katika kutatua changamoto zinazo wakabili  ikiwa ni pamoja na ; Kuendeleza elimu; ufundi stadi na kutumia teknolojia ya Habari katika kujua na kutumia fursa zilizo Tanzania.

Baadhi ya huduma na miradi imefanikishwa na tasisi hii ikiwa ni pamoja na kuelimisha,kutoa huduma za kijamii,misaada na kuazisha vikundi na miradi endelevu kwa jamii na vikundi ; Uanzishaji wa miradi ya kuingiza kipato  vijijini, Mafunzo, Ushauri na huduma za, Masoko na Habari, na Huduma za mafunzo ya ajira na kujiajiri.

Shirika linatoa huduma zake kwa kupitia ofisi zake zilizopo Moshi ,kilimanjaro,Kimara Dar es salaam na Tanga pia kwa kutumia mtandao wake wa ofisi za vikundi zilizo kzribia kila mkoa hapa Tanzania Bara .

Shirika linfanya kazi na wadau wa ndani,nje na wafadhili wanao gharamia miradi ya wanachi inayo lenga kuondoa umaskini na kukuza elimu kwa watoto na vijana, kipato kwa  vijana na akina mama,ajira kwa vijana na jamii za vijijini  na pia matumzi ya TEHAMA katika kurahisha utendaji na kupata taarifa ndani na nje ya Tanzania.

FAHAMU ZAIDI JUU YA KAZI NA MIRADI YETU TUNAYO ENDESHA NA JAMII.

MIRADI YA ELIMU MIRADI YA TEHAMA MIRADI YA AFYA NA MAJI
MIRAI YA UFUNDI NA AJIRA
MIRADI YA MAZINGIRA
MIRADI YA WATOTO MIRADI YA VIJANA

MIRADI YA AKINA MAMA