jiunge Nasi

JE UNAJUA HISTORIA YA MJI WA MOSHI –KILIMANJARO, TANZANIA?

Mji wa Moshi Ulitokea Eneo La Old Moshi, Tsudunyi Huko Mlimani Ambapo Ndipo Palikuwa Panaitwa “Moshi” Hapo Kabla.

Wakati Wageni Mbalimbali Wanakuja Kwa Wingi Sana Kilimanjaro Kuanzia Katikati Ya Karne Ya 19 Wakitokea Maeneo Ya Pwani, Ulaya, Asia na Uarabuni Waliikuta Old Moshi Ikiwa Ndio Mji Mkubwa Zaidi Kibiashara Kilimanjaro na Ikiwa Ndio Kiini Cha Utawala wa Mangi Mwenye Nguvu Zaidi na Aliyekuwa Anatawala Karibu Kilimanjaro Yote, “THE GREAT MANGI RINDI MANDARA”, Ambaye Pia Aliingia Mikataba Mbalimbali Ya Kibiashara na Mahusiano Ya Kidiplomasia na Serikali za Waingereza, Wajerumani na Hata Zanzibar.

Baada Ya Mangi Rindi Mandara Kufariki, Wajerumani Ambao Walikuwa Wameshajipanga Walibadilika na Kuanza Kuwa Wababe Wakati Huo Gavana wa Wajerumani Kilimanjaro Akiwa Dr. Karl Peters na Walijenga Kituo Cha Kijeshi Old Moshi, Hiyo Ikiwa ni Mwishoni mwa Mwaka 1891. Huo Ndio Ukawa Mwanzo wa Utawala Wao Kilimanjaro. Hata Hivyo Umangi wa Old Moshi Ulikuwa Umerithiwa na Mangi Meli Mandara Mtoto wa Mangi Rindi Mandara Ambaye Alikuwa Jeuri na Mwenye Kujiamini Sana na Hakutaka Kuwa Chini Ya Utawala wa Wajerumani, Hivyo Hakukuwa na Maelewano Mazuri Kati Yake na Wajerumani na Hata Wajerumani na Watu wa Old Moshi Kwa Ujumla Ambao Walikuwa Wajeuri Sana Dhidi Ya Ubabe wa Wajerumani.

Wakati Huo Huo Mangi Ndegoruo Marealle wa Marangu Aliimarisha Mahusiano Yake na Dr. Karl Peters Kiasi Cha Kumzawadia Binti Mrembo Sana Aliyeitwa Ndekocha na Hivyo Karl Peters Aliamua Kuhamisha Ofisi za Utawala za Wajerumani Kilimanjaro Kutoka Old Moshi, Tsudunyi Kuhamia Marangu, Lyamrakana Mwaka 1892. Lakini Karl Peters Alifanya Ukatili Mwingi Sana Pamoja na Mauaji Kilimanjaro Hususan Marangu Kiasi Cha Kuimarisha Sana Ulinzi Wake Binafsi na Hakuchukua Muda Mrefu Aliondoka Kilimanjaro. Gavan Mpya Aliyekuja Kilimanjaro Von Bulow Hakuwa na Maelewano Hata na Mangi Ndegoruo Marealle Mwenyewe Licha Ya Kuishi Marangu na Alitumia Mabavu Kujaribu Kulazimisha Kila Kitu. Ubabe Wake Ulipelekea Von Bulow Kuingia Katika Mzozo na Mangi Meli Mandara, Wakati Huo Ofisi za Utawala wa Wajerumani Zikiwa Marangu Alikozihamishia Karl Peters.

Von Bulow Aliamua Kuivamia Old Moshi Kupambana na Mangi Meli Ambaye Alionekana Ni Jeuri Sana na Asiyetishika. Von Bulow Alikusanya Majeshi Yake Pamoja na Askari Mamluki wa Kinubi Kutoka Sudan na Wengine wa Kizulu Kutoka Afrika Kusini. Mashushushu wa Mangi Meli Walikuwa Makini Kufuatilia Nyendo Zao na Mwaka 1892, Juni Waliivamia Old Moshi. Jeshi Imara Sana La Mangi Meli Lililojumuisha Askari Kutoka Old Moshi, Uru na Kilema Walijibu Mapigo Kwa Ustadi Mkubwa na Askari wa Von Bulow Waliuawa kwa Wingi Sana na Kuzidiwa, na Kupelekea Von Bulow Kukimbia Lakini Alitafutwa na Askari wa Mangi Meli Akapatikana Akiwa Amejificha Huko Kahe Naye Akauawa Pia. Baada Ya Von Bulow Kuuawa Wajerumani Wote Kilimanjaro Walikimbia na Hawakuthubutu Kurudi Kilimanjaro Kwa Karibu Mwaka na Nusu, Ni Mpaka Waliposhawishiwa Sana Kurudi Kilimanjaro, Hasa na Taasisi za Kidini.

Baada Ya Kushawishiwa Sana, Wajerumani Walirudi Kilimanjaro Mwaka 1893 Mwishoni Wakiwa na Machine Guns za Kutosha na Jeshi Imara Sana Kupambana na Majeshi Ya Wachagga. Waliingia Old Moshi Usiku na Kufanya Mashambulizi Ya Kushtukiza Kwenye Ngome Ya Mali Meli. Vita Ilipiganwa Siku Mbili Usiku na Mchana na Mangi Meli na Majeshi Yake Walizidiwa na Kuamua Kujisalimisha Ili Kuepusha Mauaji Zaidi. Mangi Meli Alipewa Masharti Ya Kutoa Malighafi na Nguvu Kazi Ya Kutosha Kujenga Kituo Kipya Cha Kijeshi Cha Wajerumani Old Moshi na Ofisi za Utawala wa Wajerumani.

Baada Ya Vita Ya Pili Kati Ya Wachagga na Wajerumani Gavana Mpya wa Wajerumani Kilimanjaro Kapteni Johannes Aliamua Kurudisha Old Moshi Ofisi za Utawala wa Wajerumani Kilimanjaro Ambazo Karl Peters Alikuwa Amezihamishia Marangu. Kapteni Johannes Alizirudisha lli Aweze Kuidhibiti Old Moshi. Hapo Ndipo Mji wa Moshi Ukarudi Upya Eneo Hilo La Tsudunyi na Ofisi za Utawala Kilimanjaro Kuanzia Mwaka 1893 – 1919.

Mwaka 1912 Reli lliyokuwa Inajengwa Ikitokea Tanga Kuelekea Kilimanjaro Ilifika Katika Tambarare za Moshi Mjini na Taratibu Ukaanza Mji Mpya Ambao Uliitwa “The New Moshi” Yaani Mji Mpya wa Moshi Kwa Sababu Mji wa Moshi Wenyewe Ulikuwa Kule Mlimani. Mwaka 1919 Ofisi za Utawala Kilimanjaro Pamoja na Taasisi Zake Kama Hospitali Ya Mawenzi, Mahakama n.k. Vilivyokuwa Old Moshi, Zilihamishiwa Huku Chini Kwenye Tambarare Ambapo Palikuwa Bado Ni Mapori Zaidi na Hakuna Hali Nzuri Sana Ya Hewa. Baadaye Ule Mji Kule Juu Mlimani Ukapewa Jina Jipya “The Old Moshi” na Mpaka Leo Panaitwa Old Moshi. Yale Majengo Yaliyokuwa Ofisi za Utawala Kule Old Moshi Sasa Hivi Ndio Majengo Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Moshi Vijijini.

Baadaye Jina La “The New Moshi” au Kwa Kijerumani “Neu Moschi” Lilikufa na Kuitwa Tu Moshi Mpaka Leo.

Huo Ndio Mji wa Moshi.

ASASI YETU INAPENDA KUWA NA WANACHAMA WENGI IKIWA NI PAMOJA NA;

MTU BINAFSIJAMII(KIJIJI,AU KATA)VIKUNDI NA ASASI VIKUNDI VYA MUUNGANO KAMA  VICOBAMASHIRIKA NA YASIYO YA KISERIKALIMAKAMPUNI NA TASISI ZA UMMA ANA BINAFSILENGO LA KUWA NA AINA HII YA WANACHAMA NI ILI KUUNGA NGUVU YA PAMOJA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO,KUBUNI FURSA NA KUSHIRKISHANA KATIKA KUPATA TAARIFA NA KUWA NA SAUTI YA PAMOJA YA KIUCHUMI,KIJAMII NA KITAALUMA